Wednesday 3 September 2014

ELIMU YA UJASIRIAMALI: UTENGENEZAJI WA MANGO PICKLES

SOMO LA SITA : UTENGENEZAJI WA MANGO PICKLES



Mango  Pickles



 MANGO  PICKLES    au    "  ACHARI  YA  EMBE  "  ni  chachandu  inayo  tumika  kunogesha  utamu  wa  chakula.   Malighafi  kuu  katika  utengenezaji  wa  "  MANGO  PICKLES "  ni  embe.

                                  MATAYARISHO

* Embe  zisafishwe  vizuri  kwa  kuosha  vizuri  kwa  kutumia  maji  masafi.
( Embe  zioshwe kabla  hazijamenywa )

* Embe  likatwe  katwe  vipande  bila  kuligusa  kokwa,  vipande  hivyo  viwekwe  kwenye  kichanja  baada  ya  kukatwa  katwa  na  vianikwe   juani  kwa  muda  wa  nusu  saa.

*  Hifadhi  embe  zako  hizo  kwenye  chombo  kisafi, kwa  muda  wa  siku  tano.


                     KUTENGENEZA  MANGO  PICKLES

* Tayarisha  nyanya  robo  kilo, menya  maganda  na  katakata  vipande  vidogo.

* Katakata  vitunguu    viwili   vikubwa.

* Chumvi   vijiko  viwili  vya  chai.

* Vinegar  _  kijiko  kimoja  cha  chai  kwa  ajili  ya  kuifanya  mango  pickle  yako  isiharibike.

* Maji  ya  limao  vijiko  viwili  vya  chai.

Tengeneza   rosti  ya  mchanganyiko  wa  malighafi  zote  zilizo  tajwa  hapo  juu. Baada  ya  kutengeneza  rosti  hiyo, chukua  vipand  vyako  vya  embe na  changanya  na  rosti  yako.

Weka  vipande  vyako  vya  embe  ndani  ya  rosti  hii, kisha  hifadhi  katika   kifungashio  kwa  ajili  ya  matumizi ..

N.B:  Kwa  kiwango  hiki  cha   rosti  una shauriwa  uweke   vipande  vya  embe  vyenye  uzito  wa  kilo  moja.  
Share:

0 comments:

Post a Comment