Wednesday, 3 September 2014

ELIMU YA UJASIRIAMALI: UTENGENEZAJI WA TOMATO SAUCE.

SOMO LA TANO : UTENGENEZAJI WA TOMATO SOUCE.

Maandalizi  ya  utengenezaji  wa  Tomato  Souce.


Tomato  Souce.

MALIGHAFI  ZINAZO  HITAJIKA  KWENYE  UTENGENEZAJI  WA  TOMATO  SAUCE.

1. Nyanya            Kg  1.5 (  Kilo  moja  na  nusu  )
2.Vitunguu  Maji.      Vitatu  vilivyo  menywa  na  kukatwa  katwa  vipande.
3. Mafuta  ya  Kupikia     Vijiko  Sita  Vya  Chakula.
4. Sukari                        Vijiko  viwili  vya  chai.
5. Citric  Acid.
6.Vinegar.                          Vijiko  viwili  vya  chai.

HATUA  ZA  KUFUATA  WAKATI  WA  UTENGENEZAJI  WA  TOMATO  SOUCE. 


Tomato  Souce  iliyo  katika  hatua  za  maandalizi 



1. Saga  mchanganyiko  wa  malighafi  zote  zilizo  tajwa  hapo  juu  kwa  pamoja  kwa  kutumia  mashine  ya  blender  mpaka  uwe  rojo  rojo.

2. Tenga  jiko  la  mkaa  lenye  moto  wa  wastani, kisha  injika kikaangio  kwenye  moto  halafu  weka  mafuta  ya  kupikia  vijiko  sita   vya  chakula.
3. Mafuta  yakianza  kuchemka , anza  kumimina  mchanganyiko  wako  huo  ndani  ya  kikaango  hicho   huku  ukiwa  una  koroga  upande  mmoja  mpaka  umalize  kuchanganya. Tumia  dakika  15  kufanya  zoezi  hili.

*  Utakapo  ona  mchemsho  wako  umeanza  kuwa  uji  uji, ipua  na  weka kwenye  chombo  safi  tayari  kwa  matumizi.
Share:

0 comments:

Post a Comment